Pwani Tribune

WhatsApp Image 2024-02-15 at 13.32.34_f2477afe

Voices from Mombasa County; Juma Mrisho.

- Advertisement -spot_img
- Advertisement -spot_img

Pwani Tribune’s ‘Voices from…’ series is a County feature of Coast Counties’ residents, in their own words. In this edition of ‘Voices from Mombasa County’, a legend…Juma Mrisho. Part of the brains behind the 1990s local hit TV show ‘Tahamaki’ on KBC. Here is his Tahamaki story (in Kiswahili)…

“Niliandika script ya kwanza mpaka ya ishirini na sita ya Tahamaki. Inspector Sikujua, Sergeant Mawazo, Corporal Kiberenge walikuwa wahusika kutoka kwa ubunifu wangu tu. Nilimuwaza Inspector Sikujua kuwa kama ‘Inspector Derrick’ wa kipindi ‘Derrick’ cha Ujerumani miaka hiyo. Kisha nikamuongezea ongezea yeye pamoja na maafisa wenzake viungo kadhaa kutoka kwengine. Sababu nilipenda sana vitabu na sinema za upelelezi na ujasusi kama vitabu vya Ian Fleming na mhusika wake 007/James Bond, pia Nick Carter na vitabu vya James Hadley Chase.”

“Nina kumbukumbu nyingi za wakati wa Tahamaki, mwanzo za uandishi. Nilikuwa nikiandika script kutumia typewriter ya zamani, zile za kelele, usiku. Kuna usiku mmoja mke wangu aliamka usiku akanifunika na bedsheet pamoja na typewriter yangu. Ili nipumzike nilale (anaeleza akicheka). Kumbukumbu nyengine ni ya uigizaji maana kando na uandishi, mimi nilikuwa jambazi kwa Tahamaki. Nakumbuka kwa tukio moja niliiga kuchinja mtu. Ilitokea kama kweli kabisa, mpaka mtoto wangu nyumbani akaniogopa ogopa kwa siku chache akifikiri lilikuwa tukio la kweli.”

“Maono na ndoto yangu ya Inspector Sikujua hayakuwa kumpandisha cheo. Alikuwa abaki hapo kwa cheo cha Inspector tu, maana juu zaidi haingekuwa sawa kumuweka kwa ‘crime scene’ akifanya upelelezi. Ata hapo kwa Inspector tayari alikuwa ni afisa na cheo chake cha kuheshimika. Hayo maono mwisho yalikatisha safari yangu na Tahamaki. Aliyecheza Inspector Sikujua hakutosheka na muda niliomtengea kwa script. Maana Inspector Sikujua alikuwa anatokea mara tatu, mwanzo wa kipindi akiwa kituoni, baadae kwa crime scene alafu mwisho kabisa akipata ukweli.”

“Tahamaki ilipokewa vizuri sana, Inspector Sikujua akiwa sura ya kipindi. Hadhi aliyowekwa Inspector Sikujua nchini ilikuwa kama ya Afisa wa Polisi wa kikweli. Basi aliyecheza Inspector Sikujua akafaulu kupata sikio la Producer, Kibwana Onguso, safari yangu nao ikaisha. Bila kujua waliifupishia maisha Tahamaki. Inspector Sikujua alipandishwa akawa Chief Inspector, Police Superintendent, mwishowe Assistant Commissioner of Police. Huo ulikuwa wakati tofauti, walionekana wameanza kuingilia kazi ya Polisi kupita kiasi. Kipindi kikakatishwa. Ijulikane kwamba kipindi kilipokea msaada mkubwa kutoka kwa Polisi nchini. Bunduki tulizokuwa tukitumia kuiga zilikuwa za kweli, ambazo Polisi wenyewe walitupatia. Lakini bila risasi na zilikuwa zimezibwa huko mbele. Kwa hiyo walikuwa na usemi kwa mambo yatakavyokwenda.”

“Hapo tu kwa Inspector kulikuwa na content ya kutosha. Nilimpangia visa kama kutekwa nyara na kutupwa Ngong majambazi wakidhani wamemuua, kumbe hajafa…wanawake wahalifu kumtilia dawa kwa kinywaji. Bora tu mwisho aibuke bingwa. Lakini mapendekezo hayo mchezaji hakuyapenda. Licha ya mambo yalivyoisha, Tahamaki nitabaki kuienzi. Hivi sasa, pamoja na Lolani Kalu tuko na CBO, Kijiweni Kaya, kukuza vipaji Pwani. Uwe muimbaji, mshairi, muigizaji, muandishi, wakaribishwa. Sisi ni vitu vyote hivyo. Tupo karibu na Msikiti Baroda, karibuni”, Juma Mrisho.

- Advertisement -spot_img
Latest news
- Advertisement -spot_img
Related news
- Advertisement -spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here